Washington. Marekani na Uingereza zakubaliana kufuta kabisa madeni ya nchi masikini.
11 Juni 2005Matangazo
Marekani na Uingereza zimekubaliana juu ya mpango wa kufuta kabisa madeni ya mataifa 18 masikini zaidi duniani ambayo mengi yao yako katika bara la Afrika.
Ikulu ya Marekani imesema kuwa nchi hizo mbili zimetayarisha utaratibu ambao utajadiliwa na mawaziri wa fedha wa kundi la mataifa tajiri yenye viwanda duniani G8 ambao wanakutana katika mji mkuu wa Uingereza, London.
Iwapo mpango huo utaidhinishwa, utaweza kufuta kiasi cha madeni yanayofikia Euro bilioni 13 kutoka mataifa hayo pamoja na taasisi zinazokopesha.
Marekani imesisitiza kutumia utaratibu huu wakati Uingereza ilitaka mataifa tajiri kuchukua jukumu la kulipa fedha hizo.