WASHINGTON: Marekani na Uingereza zakubaliana juu ya msamaha wa madeni
11 Juni 2005Matangazo
Marekani na Uingereza zimekubaliana juu ya mpango wa kufuta madeni ya nchi 18 zilizo maskini kabisa duniani ambazo nyingi zao ziko barani Afrika.
Ikulu ya Marekani imesema nchi hizo mbili zilijadili na kufikia makubaliano hayo ambayo yatajadiliwa na mawaziri wa fedha wa Kundi la Mataifa Manane yenye Maendeleo ya Viwanda Duniani wanaokutana mjini London.
Iwapo mpango huo utapitishwa utasemehe zaidi ya euro bilioni 13 za mchanganyiko wa madeni wa taasisi za mikopo kwa nchi hizo.
Marekani ilishinikiza utaratibu huo wakati Uingereza ilikuwa ikipendelea mataifa ya kitajiri yawajibike na kuyalipa madeni hayo.