WASHINGTON: Marekani imetangaza kwamba kuania kandarasi za kuijenga upya Iraq
10 Desemba 2003Matangazo
hakutazishirikisha nchi zilizopinga vita vya Iraq vilivyoongozwa na Marekani. Katika Taarifa yake ya jana,makamo waziri wa ulinzi wa Marekani Paul Wolfwitz alisema Marekani imeweka orodha ya mikataba 26 tu ya kuijenga upya Irak yenye thamani ya dala bilioni 18.6.Wolfowitz ametaja masilahi ya usalama kuwa ndio sababu ya kuzitenga nchi zilizokataa kujiunga na Marekani katika vita kama vile Ujerumani,Ufaransa na Russia.