WASHINGTON: Iran yaonywa kuhusu mradi wake wa kinuklia
29 Julai 2005Matangazo
Marekani kwa mara nyingine tena,imeionya Iran kuhusika na tangazo lake kwamba itaanzisha tena sehemu ya mradi wake wa kinuklia.Msemaji wa Ikulu mjini Washington amesema,matokeo ya hatua hiyo huenda ikawa ni Iran kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na Umoja wa Mataifa.Serikali ya Marekani inaituhumu Iran kuwa inataka kutengeneza silaha za kinuklia.Lakini serikali ya Teheran inasisitiza kwamba inahitaji yuraniumu halisi kupata nishati.