WASHINGTON: Hakuna ratiba ya vikosi kuondoka Iraq
14 Septemba 2005Matangazo
Rais George W.Bush wa Marekani na Rais wa Iraq Jalal Talabani,wamekataa kupanga tarehe maalum ya
kuvihamisha vikosi vya Kimarekani kutoka Iraq.Lakini,katika mkutano wao na waandishi wa habari,Talabani alieleza matumaini yake kuwa hadi mwisho wa mwaka ujao,hakutokuwepo haja ya kuwa na vikosi vingi vya Kimarekani kama hivi sasa.Rais Talabani alinukuliwa na gazeti la Washington Post siku ya jumanne,akisema kuwa hadi wanajeshi 50,000 wataweza kuondoka Iraq ufikapo mwisho wa mwaka huu.Lakini,kile alichotamka katika mkutano na waandishi wa habari,kuhusu ripoti hiyo ni kwamba ratiba kuhusu tarehe ya kuondoka kwa vikosi vya Kimarekani,haiwezi kupangwa kwa sababu jambo hilo litawasaidia magaidi tu.