Washington . Bush ailaumu Syria na Iran kwa kuunga mkono magaidi.
7 Oktoba 2005Rais wa Marekani George W. Bush amesema kuwa wapiganaji wa Kiislamnu wanataka kuanzisha vita dhidi ya ubinadamu. Katika kilichoelezwa kuwa ni hotuba muhimu, Bush ameilaumu Syria na Iran kwa kuwaunga mkono magaidi.
Bush pia amekataa wazo kuwa kuwapo kwa majeshi ya Marekani nchini Iraq kunaamsha hisia za chuki dhidi ya Marekani.
Amewataka Wamarekani kuwa watulivu na ameahidi kupata ushindi katika vita vya Iraq. Hotuba hiyo inakuja katika wakati ambao uungwaji mkono wa vita dhidi ya Iraq na wananchi unazidi kupungua. Uchunguzi mmoja wa maoni uliofanywa mwishoni mwa mwezi uliopita unaonyesha kuwa ni kiasi cha asilimia 32 tu ya Wamarekani wanaunga mkono jinsi utawala wa Bush unavyolishughulikia suala la Iraq.