Washington/Baghdad Wananchi wa Iraq wanasherehekea kukamtwa mtawala wa zamani Sadam Hussein.
15 Desemba 2003Matangazo
Naiongozi toka kila pembe ya dunia wamefurahishwa na kupumua.Wameelezea matumaini yao kuona matumizi ya nguvu yanamalizika.Rais George W. Bush wa Marekani amesema Sadam Hussein atafikishwa mahakamani.Amewataka wananchi wa Iraq washirikiane,walaani matumizi ya nguvu na kuijenga upya nchi yao.Waziri wake wa ulinzi Donald Rumasfeld amesema kukamtwa Sadam Hussein kumehitimisha "utawala wa kigaidi"."Enzi za utawala wakiimla wa matumizi ya nguvu imemalizika"-amesema hayo waziri wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld.Akizungumza na kituo cha televisheni cha CBS waziri Rumsfeld amesema Sadam Hussein atatendewa sawa na mfungwa wa vita kuambatana na makubaliano ya Geneva.Mshauri wa rais Bush katika masuala ya usalama Condoleesa Rice anahoji hata hivyo kukamatwa Sadam Hussein hakumaanishi kupungua matumizi ya nguvu dhidi ya vikosi shirika nchini Iraq.Amesema na hapa tunanukulu:" kukamatwa Sadam Hussein sio mwisho wa mapambano ya kuikomboa Iraq-"Mwisho wa kumnukulu.Washirika wa Marekani katika vita vya Iraq nao pia wameshangiria.Waziri mkuu wa Uengereza Tony Blair ametoa mwito wa kusahauliwa yaliyopita.Amesema ni wachache tuu nchini Iraq wanaomlilia Sadam Hussein na kutaka arejee madarakani.Nae waziri mkuu wa Italy amefanya mzaha na kusema "kwakua silaha ya maangamizi imeshagunduliwa,watu wanabidi wasahau yaliyopita."Mwisho wa kumnukulu.
Matangazo