Washington/Baghdad: Rais wa zamani wa Iraq Sadam Hussein atahukumiwa ...
10 Januari 2004Matangazo
kama mfungwa wa kivita.Habari hizo zimetangazwa na wizara ya ulinzi ya Marekani.Kanuni za mfungwa wa kivita zina umuhimu mkubwa katika kuhakikisha mtawala huyo wa zamani wa Iraq hanyimwi haki zake akiwa kifungoni au atakapofikishwa mahakamani.Waziri wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld aliahidi mwezi uliopita,Sadam Hussein atalindwa na mkataba wa Geneva..Mahala anakoshikiliwa Sadam Hussein lakini hakujulikani.Hakimu Dara Nourredine,mwanachama wa serikali ya mpito nchini Iraq anaashiria Sadam Hussein atafikishwa mahakamani nchini Iraq kwenyewe katika kipindi cha miezi sita ijayo.Amesema kesi hiyo itaendeshwa na mahakimu wa kutoka Iraq wakisaidiwa na wanasheria wa kutoka nchi za nje.Kwa maoni yake Sadaam Hussein atahukumiwa kwa makosa ya kuwatumilia gesi za sumu wakurd wa Halabja katika mwaka 1988 na kuwakandamiza wakaazi wa madhehebu ya shiya katika miaka ya 80 na 90.Wakati huo huo Marekani inasema haina ushahidi wowote kama silaha za maangamizi za Iraq zimefichwa nchini Syria.