WASHINGTON: Afghanistan na Pakistan zishirikiane zaidi
28 Septemba 2006Matangazo
Rais George W.Bush wa Marekani ametoa mwito kwa Afghanistan na Pakistan kushirikiana bora zaidi kupiga vita ugaidi.Alipokutana na marais Hamid Karzai wa Afghanistan na Pervez Musharraf wa Pakistan,katika Ikulu mjini Washington,Bush alisema majirani hao wawili wanakabiliwa na changamoto za aina moja.Bush akaendelea kusema lazima ihakikishwe kuwa kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda Osama Bin Laden anafikishwe mahakamani.Majuma yaliopita,Karzai na Musharraf wamekuwa wakilaumiana kutochukua hatua kali za kutosha kupiga vita ugaidi na kupambana na Wataliban waliopata nguvu upya.Inadhaniwa kuwa Bin Laden amejificha karibu na mpaka wa Afghanistan na Pakistan.