Wasaidizi wa Kijerumani wawawili Iran:
27 Desemba 2003Matangazo
FRANKFURT MAIN: Hivi leo zimeanza kwa kasi juhudi za kimataifa za kuwapatia misaada watu waliokubwa na maafa ya mtetemeko wa ardhi nchini Iran. Mjini Kerman iliwasili ndege yenye makundi ya mabingwa wa kuokoa watu kutoka Shirika la Misaada ya Kiufundi la Kijerumani pamoja na mashirika mengine ya Kijerumani. Mjini Berlin, Wizara ya Mambo ya Nje imeunda kundi la mabingwa la ushauri wa dharura. Iran imeahidiwa misaada pia na nchi nyingine kama vile Marekani, Ufaransa, Uingereza na Urusi. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran Jahanbash Chanshani alisisitiza kuwa nchi yake itapokea misaada hiyo kutoka nchi zote nyingine, pamoja na Marekani, isipokuwa kutoka utawala wa Kizayuni wa Israel. Bwana Chanshani alisema misaada ya dharura inayohitajiwa ni mitambo inayotumia ufundi wa kuwatafuta watu waliopotea walionusurika pamoja na madawa, mablangeti, mahema na nyumba zinazoweza kuezekwa haraka kwa watu waliopotelewa na maskani yao.