Waromania washiriki duru ya pili ya uchaguzi wa rais
18 Mei 2025Uchaguzi huo wenye maslahi makubwa huenda ukaamuwa mkondo wa saisa za kikanda za nchi hiyo mwanachama wa Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Kujihami ya NATO. Kinyang'anyiro hicho ni kati ya kiongozi anayepigiwa upatu George Simion, wa muungano wa siasa kali za mrengo wa kulia, Alliance for the Unity of Romanians - AUR mwenye umri wa miaka 38 na Meya wa sasa wa mji mkuu, Bucharest, Nicusor Dan.
Unafanyika baada ya kufutwa kwa uchaguzi wa awali kuitumbukiza Romania katika mgogoro mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika miongo kadhaa. Hali ya kisiasa ya Romania ilivurugika Disemba mwaka jana wakati mahakama ya juu ilipobatilisha uchaguzi baada ya mgombea wa siasa kali za mrengo wa kulia Calin Georgescu kuongoza katika duru ya kwanza ya uchaguzi, kufuatia madai ya ukiukaji wa uchaguzi na kuingiliwa na Urusi, ambayo Moscow ilikanusha.