Raia wa Romania wapiga kura kumchagua Rais
4 Mei 2025Iwapo kiongozi huyo atachaguliwa hali hiyo itasababisha kuongezeka kwa makundi ya watu wanaozingatia utaifa katika nchi za Umoja wa Ulaya kwa kufuata mtindo wa uongozi wa Rais wa Marekani Donald Trump.
George Simion, wa chama cha kisiasa cha AUR, mwenye umri wa miaka 38, anapinga msaada wa kijeshi kwa nchi jirani ya Ukraine na pia ni mkosoaji wa uongozi wa Umoja wa Ulaya na anasema anaambatana na mtazamo na msimamo wa rais wa Marekani wa kuirudishia hadhi ya nchi yake maarufu kama (MAGA).
Waromania takriban milioni 1.98 sawa na asilimia 11 waliosajiliwa kupiga kura, walikuwa wamepiga kura kufikia saa moja asubuhi. Zoezi la kupiga kura litamalizika saa 9 alasiri kwa saa za Ulaya ya Kati na kufuatiwa mara moja na zoezi la kuhesabu kura. Matokeo ya awali yanatarajiwa kutolewa baadaye jioni.