WAPINZANI WASHAMBULIWA IRAQ
24 Desemba 2003Matangazo
BAGHDAD: Eneo la kusini mwa Baghdad limekumbwa na miripuko ya nguvu.Wakaazi wa eneo hilo wamesema wanajeshi wa Marekani wanapambana vikali na watu wenye bunduki.Kwa mujibu wa wakaazi hao ndege za Kimarekani pia zimeshiriki katika mapigano hayo.Msemaji wa vikosi vya Marekani mjini Baghdad amethibitisha kuwa opresheni ya kijeshi inaendelea.Akasema kuwa hiyo ni sehemu ya opresheni yenye lengo la kuwafyeka wapinzani wanaovishambulia vikosi vilivyoikalia Iraq chini ya uongozi wa Marekani.