Wapiganaji waua watu 35 mashariki mwa Kongo
8 Machi 2025Takriban watu 35 wameuawa wakati wanamgambo wanaoiunga mkono serikali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waliposhambulia kijiji kimoja mashariki mwa nchi hiyo, hayo yamesemwa na vyanzo vya ndani na usalama hapo jana.
Mashambulizi hayo yaliyofanywa na wapiganaji wanaojiita wazalendo yamefanyika siku ya Alhamisi katika kijiji chaTambi kilichopo katika eneo la Masisi katika jimbo la Kivu Kaskazini na ambalo kwa sasa linadhibitiwa na kundi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda.
Soma zaidi. Rais wa zamani wa DRC aanzisha mazungumzo kuhusu mustakabali wa nchi hiyo
Vyanzo vya usalama vimeliambia shirika la habari la AFP kwamba watu 35 wameuawa huku mashuhuda na vyanzo vya ndani vikisema huenda zaidi ya watu 40 wamekufa kutokana na mashambulizi hayo.
Makundi tofauti yanayounda wanamgambo hao, ambao wanapigana pamoja na jeshi la Kongo dhidi ya M23 yamekuwa yakishutumiwa mara kadhaa kwa kushambulia raia.