Zaidi ya wapiganaji mia sita wa Maimai wamesalimisha silaha zao na kuzikabidhi kwa mkuu wa majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo katika wilaya ya Beni na kutangaza utayari wao wa kuhudumu katika jeshi la taifa. Wapiganaji hao wanafanya hivyo siku moja kabla ya kuanza operesheni kabambe dhidi ya makundi ya waasi, likiwemo kundi kubwa kuliko yote la ADF kutoka Uganda.