Wapiganaji wa itikadi kali wawauwa wakulima 14 Nigeria
27 Aprili 2025Matangazo
Timita ameongeza kuwa wapiganaji hao walifanya shambulizi hilo kutoka kijiji cha karibu cha Vlei ambapo wanaendesha oparesheni zao.
Ameongeza kuwa wakulima hao walikuwa wakiliandaa shamba lao jana Jumamosi karibu na mji wa Pulka wilayani Gwoza kwa ajili ya msimu ujao wa upanzi walipovamiwa.
Watu wenyei silaha wamewaua takribani watu 56 Nigeria
Chifu huyo amesema kuwa vikosi vya uokoaji, vikiambatana na wanajeshi, vilikuwa vikiendeleza juhudi zao kutafuta miili zaidi.
Mara kwa mara, mji huo ulio karibu na mpaka na Cameroon umekuwa ukishambuliwa namakundi ya watu wenye silaha.