Gaza yashuhudia Eid kwa mashambulizi makali ya Israel
30 Machi 2025Mashambulizi hayo yametokea wakati huu ambao waislamu wanasherehekea siku ya kwanza ya Eid Ul Fitri baada ya kumalizika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Shambulizi hilo limetokea wakati pande zote mbili hasimu wanamgambo wa Hamas na Israel wakithibitisha kupokea pendekezo jipya kutoka kwa wapatanishi likinuiwa kusitisha mashambulizi wakati wa siku kuu.
Makubaliano ya awali yaliotoa nafasi ya utulivu mjini Gaza, yalikiukwa machi 18 wakati Israel ilipoanzisha mashambulizi mapya ya ardhini na angani katika maeneo ya wapalestina.
Wimbi jipya la mashambulizi ya Israel huko Gaza laua watu 921
Mashambulizi ya hayo yametokea wakati wapatanishi ikiwa ni pamoja na Misri, Qatar,na Marekani wakiendelea na juhudi za kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano na kufikia pia makubaliano ya kuwaachia mateka wa Israel ambao bado wanashikiliwa na hamas mjini Gaza.