Wapalestina kiasi 10 wauwawa Gaza
16 Aprili 2025Watu wasiopungua 10 wameuwawa katika shambulizi la Israel lililoilenga nyumba moja huko Kaskazini mwa Gaza. Ripoti hiyo imetolewa na shirika la habari la Palestina WAFA, ambalo pia limenukuu vyanzo vya madaktari vilivyosema kwamba watu wengine wengi wamejeruhiwa.Soma pia: Misri na Qatar zawasilisha pendekezo jipya kwa Hamas
Jeshi la Israel limesema linachunguza ripoti hiyo. Shirika la WAFA limechapisha picha zinazotajwa kuonesha athari za shambulio hilo lililofanywa usiku wa kuamkia leo katika wilaya iliyoko mashariki mwa Gaza City.
Jeshi la Israel limekuwa likiendesha operesheni iliyoianzisha kwenye eneo hilo mwishoni mwa juma lililopita kutanuwa kile inachokiita''eneo la usalama na raia wametakiwa kuondoka kwenye eneo hilo.Soma pia: Hamas yatathmini pendekezo jipya la kusitisha mapigano Gaza
Leo waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz amesema vikosi vyake vitabakia milele kwenye maeneo hayo yanayoitwa''maeneo ya usalama'' katika Ukanda wa Gaza,Lebanon na Syria, kauli ambayo huenda ikazidisha hali ya mkanganyiko katika mazungumzo na Hamas kuhusu usitishaji mapigano na kuachiliwa kwa mateka.