Wapalestina 38 wauwawa wakitafuta chakula Gaza
16 Juni 2025Matangazo
Wizara ya afya katika Ukanda wa Gaza imesema Wapalestina 38 wameuwawa kwa kufyetuliwa risasi katika mashambulio mapya yaliyofanyika kwenye maeneo ya vituo vya kugawa chakula, kusini mwaGaza.
Jeshi la Israel bado halijatowa tamko kuhusu mashambulizi hayo. Idadi ya Wapalestina waliouwawa leo ndiyo kubwa zaidi kuwahi kuonekana katika matukio hayo ya karibu kila siku ya ufyetuaji risasi dhidi ya Wapalestina wanaotafuta chakula kwenye vituo vinavyodhibitiwa na jeshi la Israel, ndani ya Gaza.