Wapalestina 28 wauawa kwenye shambulizi la Israel Gaza
12 Julai 2025Maafisa hao wamesema kuwa watoto hao na wanawake wawili ni miongoni mwa watu 13 waliouawa huko Deir al-Balah, katikati mwa Gaza, baada ya mashambulizi hayo ya Israel kulenga eneo hilo kuanzia jana Ijumaa jioni.
Kulingana na hospitali ya Nasser, watu wengine wanne waliuawa katika mashambulizi karibu na kituo cha mafuta na wengine 15 katika eneo la Khan Younis, kusini mwa Gaza.
Watu 800 wauawa Gaza tangu Mei wakijaribu kupata msaada
Kupitia taarifa, jeshi la Israel limesema kuwa katika muda wa saa 48 zilizopita, wanajeshi walishambulia takriban maeneo 250 katika Ukanda waGaza, ikiwa ni pamoja na wapiganaji, miundombinu, maeneo ya kuhifadhia silaha, na mahandaki.
Hata hivyo jeshi la Israel halikujibu mara moja ombi la tamko kutoka kwa shirika la habari la AFP kuhusiana na vifo vya raia.