Wapalestina 25 wauawa wakati wa usambazaji wa msaada Gaza
1 Juni 2025Maafisa wa afya na mashuhuda wamesema vikosi vya Israeli vilifyatua risasi kwenye umati wa watu waliokuwa karibu kilomita moja kutoka kituo cha msaada kinachoendeshwa na shirika linaloungwa mkono na Israeli. Jeshi lilitoa taarifa fupi likisema kwa sasa halijui idadi ya waliojeruhiwa katika tukio hilo la ufyatuaji risasi lililofanywa na askari wa Israel katika kituo cha usambazaji wa Misaada ya Kibinadamu. Limesema suala hilo bado linachunguzwa."
Soma pia:Mpango wa Marekani juu ya misaada ya kiutu Gaza wapingwa
Taasisi hiyo imesema katika taarifa kwamba ilitoa msaada "bila tukio lolote" mapema Jumapili na imekanusha taarifa za awali za machafuko na milio ya risasi karibu na vituo vyake, ambavyo vipo katika maeneo ya kijeshi ya Israeli. Sio rahisi kuthibitisha ripoti hizo kutokana na changamoto za kuyafikia maeneo hayo.
Maafisa katika hospitali ya karibu inayosimamiwa na Shirika la Msalaba Mwekundu walisema takriban watu 25 waliuawa na wengine 175 walijeruhiwa, bila kusema ni nani aliyewafyatulia risasi. Viongozi hao walizungumza kwa sharti la kutotajwa majina yao kwa sababu hawaruhusiwi kuzungumza na wanahabari.