Wapalestina 16 wauawa wakisaka chakula Gaza
5 Agosti 2025Matangazo
Mashahidi na maafisa wa afya kwenye Ukanda huo wamesena 16 waliuawa karibu na kituo cha mpakani cha Zikim, ambacho ni lango kuu la kupitishia misaada kuingia Gaza.
Hospitali ya Shifaa kwenye eneo la Gaza City imechapisha orodha ya watu wengine 130 waliojeruhiwa kwenye mkasa huo.
Mzingiro wa kijeshi wa Israelumesababisha iwe shida kwa misaada kuwafikia mamilioni ya watu wanaoteseka kwa njaa na hali ngumu ya kibinaadamu kwenye Ukanda huo.
Mamia ya Wapalestina wameuawa tangu mwezi Mei wakati wakielekea kwenye maeneo ya mgao wa chakula yanayoendeshwa na Wakfu wa Kibinaadamu wa Gaza, GHF, shirika linaloungwa mkono na Israel na Marekani, na ambalo Umoja wa Mataifa unalikosowa kwa kutokuzingatia misingi na sheria za kibinaadamu kwenye shughuli zake.