Ushiriki wa wanawake katika taasisi za utawala na miradi ya ujasiriamali bado ni mdogo nchini Burundi. Mkuu wa kitengo cha mikopo ya miradi ya ujasiriamali anasema kati ya miradi 4,700 waliyopokea tangu 2021, miradi 700 ndio ilikuwa ya wanawake. Wizara ya mshikamano kitaifa imehimiza wanawake kujitokeza kupiga kura na kuwania uongozi kwenye uchaguzi wa mwezi Julai. Amida ISSA alituandalia ripoti.