Makala ya Wanawake na Maendeleo inalimulika kundi la wanawake wa nchini Kenya walioungana kwenye mpango wa kuzalisha dawa ya mbu, kutoka kwa mashamba yao ya pareto na kuiuza kwenye masoko ya nje ya nchi ikiwa ni pamoja na Japan. Wakio Mbogho amewatembelea na kuandalia makala hiyo.