Wanawake 162 wakombolewa kwenye biashara ya ukahaba
22 Julai 2025Matangazo
Maafisa nchini Uhispania wamewakombowa wanawake 162 waliokuwa wakilazimishwa kufanya kazi ya ukahaba katika maeneo ya kitalii ya Valencia, Alicante, Malaga na Murcia.
Polisi ya Uhispania imesema, wanawake hao walikuwa wakitumikishwa na genge la wanaoendesha biashara haramu ya kusafirisha binadamu. Kwa mujibu wa polisi watu 39 wamekamatwa huku washukiwa tisa katika kadhia hiyo wakiwekwa rumande.
Wengi wa wahanga wanatajwa kutokea mataifa ya Amerika Kusini. Taarifa zinasema wanawake hao ambao hawana vibali vya ukaazi wala vya kuruhusiwa kufanya kazi Uhispania, walikuwa wakiwekwa kwenye mazingira mabaya, kunyimwa uhuru na wakilazimishwa kukabidhi malipo waliyopokea kwa magenge hayo.