Wananchi wa Arusha wajitokeza kwa wingi kupiga kura
Elizabeth Shoo25 Oktoba 2015
Mgombea wa urais kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa, amepiga kura yake nyumbani Monduli. Wakazi wa Arusha wameelezea kufurahia ulinzi katika vituo vya kupigia kura.
Mamia kwa mia ya watu walijihimu mapema kuwahi katika vituo vya kupiga kura katika majimbo mbalimbali ya uchaguzi na kushuhudia kasoro za kawaida ambazo zilirekebishwa na wasimamizi wa vituo mbalimbali na hatimaye wapiga kura walianza zoezi kwa amani na utulivu.