Wanamgambo wanne wa Taliban wauawa Afghanistan:
28 Desemba 2003Matangazo
KABUL: Huko Afghanistan Kusini ya Mashariki wanajeshi wa Kimarekani wamewauwa wanamgambo wanne wa Taliban. Msemaji wa wanajeshi wa Kimarekani aliarifu mjini Kabul kuwa wanamgambo hao walimpiga risasi na kumwuwa mtu mmoja aliyewaonya wanajeshi wa Kimarekani kwamba watashambuliwa. Baada ya hapo yalitokea mapigano makali ya risasi karibu ya mji wa Chost. Inasemekana mtu huyo aliyeuawa alikuwa mtumishi wa Shirika la Kijasusi la Afghanistan. Wanajeshi wa Kimarekani wanakisia kuwa katika mkoa huo unaopakana na Pakistan huko Afghanistan Kusini-Mashariki wangaliko wanamgambo miya kadha wa Taliban na Al Qaida.